Eido al-Ghadir
Mada | Uteuzi wa Ali bin Abi Talib Kuwa Khalifa Baada ya Mtume (s.a.w.w) |
---|---|
Wakati wa Kufanyika | Terehe 18 Dhul-Hijja |
Asili Kihistoria | Hijjatul Wadaa |
Dua |
Eid al-Ghadir (Kiarabu: عيد الغدير) ni miongoni mwa sikukuu kubwa za Mashia. katika siku ya 18 ya Dhul al-Hijjah, mwaka wa kumi hijiria Mtume Muhammad (s.a.w.w) alimteua Imam Ali(a.s) kuwa khalifa baada yake. Tukio la Ghadir lilitokea katika Hija ya mwisho ya Mtume katika eneo linaloitwa Ghadir Khum.
Katika vitabu vya mashia, siku hii imetajwa kwa majina mbalimbali kama vile (عیدُاللهِ الاکبر) Sikukuu kubwa ya Mwenyezi Mungu, eid ya ahlubaiti ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), na (اشرف الاعیاد) eid bora zaidi. Mashia wote duniani huheshimu na kusherehekea siku hii na katika nchi ya Iran Eid al-Ghadir ni likizo rasmi.
Tukio la Ghadir
Mnamo tarehe 24 au 25 Dhul-Qa'dah mwaka wa 10 Hijiria, Mtume Muhammad(s.a.w.w) akiongozana na maelfu ya waislamu walitoka Madina kuelekea Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada za Hija.[1] Hija hi ilitambulika kama Hajjat al-Wida' (حجة الوداع) hija ya mwisho ya mtume.[2] Shughuli za Hija zilipoisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) na maswahaba zake walitoka Makka na kuelekea Madina, na mnamo tarehe 18 Dhul-Hijjah, walifika eneo linaloitwa Ghadir Khum,[3] katika eneo hili Jibril akateremsha Aya ya Tabligh kwa Mtume (s.a.w.w) iliyomuamuru Mtume wa Mwenyezi Mungu kumtambulisha Imam Ali (a.s) kwa watu kama wasii na Khalifa baada yake.[4]
Khutba ya Ghadir
- Makala Asili: Khutba ya Ghadir
Kwa mujibu wa hadithi zilizopokelewa katika vitabu mbalimbali, Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliwakusanya watu katika eneo la Ghadir Khum na akainua mkono wa Imam Ali (a.s) ili kila mtu aweze kumuona na akasema: "Enyi watu, je, mimi sio bora zaidi kwenu kuliko nafsi zenu?" Watu wakajibu: Ndio, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. mtume akasema: "Mwenyezi Mungu ndiye mlezi wangu na mimi ni mlezi wa waumini na nina mamlaka zaidi juu yao kuliko wao wenyewe. Kwahiyo, yeyote ambaye mimi ni kiongozi wake, basi Ali pia ni kiongozi wake." Mtume(s.a.w.w) alirudia sentensi hii mara tatu na kusema:
Ewe Mola mpende na umlee yeyote anayempenda Ali na kumchulia kama mlezi wake, na mchukie yeyote anayemchukulia kuwa ni adui wake, na msaidie yeyote anayemsaidia, na mtelekeze yeyote atakaemuacha.
Kisha akasema: Waliopo wafikishe ujumbe huu kwa wasiokuwepo.[5]
Eid al-Ghadir katika Hadithi
Imepokewa katika vitabu vya نisunni kwamba mwenye kufunga swaumu wiki ya 18 Dhul-Hijjah, Mwenyezi Mungu atamwandikia malipo ya swaumu ya miezi sita, na siku hii ni ndio siku ya Eid al-Ghadir .[6]
Mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema: "Siku ya Ghadir ni siku kuu bora zaidi kwa ummah wangu na ni siku ambayo Mwenyezi Mungu aliniamrisha nimchague ndugu yangu Ali bin Abi Talib kuwa mshika bendera wa ummah wangu ili aongoze ummah wa kislam baada yangu. Na katika siku hiyo Mwenyezi Mungu aliikamilisha Dini ya kislam, na kukamilisha baraka zake juu ya Ummah wangu, na akaufadhilisha Uislamu kuwa dini kwao."[7]
imepokelewa kutoka Kwa Imamu Sadiq (a.s) akisema: "Siku ya Ghadir ni Eid kuu ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hakumtuma mtume isipokuwa anaifanya Siku hiyo kuwa ni Eid na kutambua ukubwa wake, na jina la siku hii huko mbinguni ni siku ya ahadi na makubaliano duniani, siku ya Muungano thabiti baina ya watu wote."[8] Katika riwaya nyingine, Imamu Sadiq (a.s) anaichukulia Eid ya Ghadir kama Eid kubwa na yenye heshima zaidi ya waislamu, ambayo inastahiki katika siku hiyo kushukuriwa kwa Mwenyezi Mungu na watu wafunge kwa kushukuru, kwani kufunga siku hii ni sawa na miaka sitini ya ibada.[9]
Vilevile imepokelewa kutoka Kwa Imamu Reza (a.s) akisema: "Siku ya Ghadir ni mashuhuri zaidi miongoni mwa watu wa mbinguni kuliko watu walioko ardhini… Lau watu wangejua thamani ya siku hii, bila shaka, malaika wangepeana nao mikono mara kumi kwa siku."[10] Historia ya sikukuu ya Ghadir
Hassan bin Thabit alikuwa mtu wa kwanza kusimama mbele ya Mtukufu Mtume Muhammad(s.a.w.w) siku ya Ghadir na kuadhimisha siku hii miong,oni mwa umati wa waislamu waliokuwepo katika eneo hilo na akasoma mashairi yake aliyoyaandika kwa idhini ya Mtume[11]. Fayaz bin Muhammad bin Umar Tusi anasimulia hadithi kwamba Imam Reza(a.s) alikua akisherehekea siku ya Ghadir . Alikua akiwaalika kundi la masahaba zake kwa ajili ya kufuturu, na alikua akitoa zawadi nyingi kama vile chakula, nguo na hata viatu na pete kwa familia zao.[12]
Kwa mujibu wa Amini, mwaka wa 259 Hijiria, Ahmad bin Is’haq Qomi, mwakilishi wa Imamu Hasan Askari (a.s), aliokuwepo katika mji wa Qom alifanya sherehe nyumbani kwake katika siku ya Ghadir [13] Masoudi (aliyefariki mwaka 346 AH), mwanahistoria wa karne ya nne hijiriya, aliandika katika vitabu vyake vya al-Tanbiyyah na al-Ashraf kwamba watoto na mashia wa Imam Ali (a.s) wanasherehekea siku hii[13]Kuleini (aliyefariki mwaka 328 AH), Msomi wa hadithi wa karne ya 4, pia Ameelezea sherehe za mashia. Katika wiki ya Ghadir.[14]
Ili kuonyesha umuhimu wa Eid hii, serikali ya Al-Buyeh iliitangaza siku hii kuwa sikukuu ya umma na kuhimiza taasisi za serikali na watu wote kuandaa sherehe na kupamba miji.[15] Walitumia ngoma na baragumu katika sherehe hizi. Walitembelea maeneo matakatifu na kuswali swalah ya Eid na kuchinja ngamia, na wakati wa usiku walikuwa wakiwasha moto mkumbwa na kusherehekea.[16] Gardizi alichukulia siku hii kuwa miongoni mwa siku kuu kumbwa ya kiislamu haswa wafuasi wa ahlulbait (a.s).[17]
Huko Misri, makhalifa wa Fatimiyah waliirasimisha Eid ya Ghadir , na nchini Iran, tangu 907 AH wakati Shah Ismail Safavi alipochukua madaraka, aliifanya siku ya Ghadir kuwa likizo rasmi. Mnamo mwaka wa 487 Hijiria, kiapo cha utii kilitolewa na Mustali bin Mostanser (mmoja wa watawala wa Misri) katika siku ya Ghadir.[18] Eid al-Ghadir ni sikukuu rasmi nchini Iran.[19] Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya majimbo ya Iraq kama vile Karbala, Najaf na Dhiqar wameifanya wiki ya Ghadiri kuwa likizo rasmi.[Inahitaji chanzo] Mashia pia huona usiku wa Ghadir kuwa ni usiku wenye fadhila kumbwa na hukesha usiku huo Kwa kufanya ibada mbalimbali.[20]
Matendo ya Siku ya Ghadir
- kufunga
- kuoga (kufanya ghusli)
- Kusoma ziarat Aminullah
- kusoma dua ya nudba
- Kusema maneno yafuatayo pindi wnapokutana na waumine:
اَلحمدُ لِلهِ الّذی جَعَلَنا مِنَ المُتَمَسّکینَ بِولایةِ اَمیرِالمؤمنینَ و الائمةِ المَعصومینَ علیهم السلام - Kuvaa nguo nzuri
- Kujipamba
- kutumia manukato
- kutembelea ndugu na jamaa
- Kuwalisha waumini
- kusoma ziyara ya Ghadiriya
- kusali swala ya Eid Ghadir. Swala hii inasaliwa wakati wa mchana. Swala hii ina rakaa mbili, na katika kila rakaa,baada ya Suraht al-Hamd inasomwa suratul al-Ikhlas mara 10, ayat al-kursi mara 10 na surat al-Qadr mara 10.Kuna ikhtilafu baina ya mafakihi kuhusu kujuzu na kutokujuzu kwa kuswali swala hii kwa jamaa.
Rejea
- ↑ Ṭūsī, Tahdhīb al-Aḥkām, 1407 H, juz. 5, uk. 474; Twabari, Tarikh al-umam wa al-Muluk,1387 H, juz. 3, uk. 148.
- ↑ Zarqani, Sharh al-Zarqani,1417 H, juz. 4, uk. 141 ; Tari, Taamuli dar Tarikh-e wafat-e Payambar, uk. 3
- ↑ Ya'qubi, Tarikh al-Ya'qubi, juz. 2, uk. 112
- ↑ Iyazi, Tafsir Qur'an al-Majid,1422 H, hlm. 184 ; Ayashi, Tafsir Ayasyi, juz. 1, uk. 332
- ↑ Ibnu Astsir Usd al-Ghabah, 1409 H, juz. 3, uk. 608 ; Kuleini, al-Kafi,1407 H, juz. 1, uk. 295 ; Baladzuri, Ansab al-Asyraf,1417 H, juz. 2, uk. 110-111 ; Ibnu kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah,1407 H, juz. 7, uk. 349
- ↑ Sheikh Swaduq, al-Amāli, uk. 188.
- ↑ Hur Amili, Wasail al-Shiah,1416 H, juz. 10, uk. 89.
- ↑ Hur Amili, Wasail al-Shiah,1416 H, juz. 8, uk. 89.
- ↑ Thusi, Tahdzib al-Ahkam,1365 S, juz. 6 uk. 24.
- ↑ Naswibi, Matwalib al-Suul, 1419 H, uk. 64
- ↑ Naswibi, Matwalib al-Suul, 1419 H, uk. 79
- ↑ Ibnu Khalqan, Wafiyat al-A'yan, juz. 17, uk. 180
- ↑ Sayyied Ridhwa, Khaswaiswu al-aimah, 1406 H, uk. 42
- ↑ Majlisi, Biharul-anuar, juz. 95, uk. 322
- ↑ Masoudi, Tanbih wal-ishraf, 1357 H, uk. 221
- ↑ Kulein, al-Kāfi, juz. 4, uk. 149.
- ↑ Ibnu kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, 1408 H, juz. 11, uk. 276
- ↑ Ibnu jawzi, Al-muntadhwim fi tarikh al-umami wa al-muluk, 1412 H, juz. 15, uk. 14
- ↑ Gardizi, Zainul-akhbar, 1363 S, uk. 466
- ↑ Nikzaad Tehran wa Hamze, "Tashayuh wa tarikh ijtimay iraniyan dar asri safavi", uk. 131