Hadithi ya "رفع القلم" (Rufu'a Al-Qalamu)
Taarifa za Hadithi • Mada: Kuturekodiwa kwa madhambi ya Mashia katika siku ya tisa ya Rabiul Awwal. • Mapokezi: Imepokewa kutoka kwa Imamu Hadi (a.s), Imamu Jawad (a.s), na Mtume (s.a.w.w). • Msimulizii Mkuu: Yahya bin Muhammad bin Khurayj Al-Baghdadi. • Uhalali wa Sanad Yake: Haikubaliki. • Vyanzo vya Kishi'a: Al-Mukhtasar, Fawaid Al-Fawaid, na Bihar Al-Anwar.
Hadithi Mashuhuri
Hadithi ya "رفع القلم" (Rufu'a Al-Qalamu): Ni Hadithi inayonasibishwa na bwana (s.a.w.w), nayo ni ile Hadithi isemayo kwama; Ifikapo siku ya tisa ya mwezi wa Rabi' al-Awwal kalamu yenye kurekodi madhambi husimama na kutorekodi madhambi ya Mashia. Baadhi ya watu, wakitumia Hadithi hii kama hoja na kisngizio cha matendo yao, husimama na kuadhimisha siku hii, wakiamini kwamba, siku hii ndiyo siku aliyo uawa Omar ibn al-Khattab. Katika maadhimisho yao hayo, utawaona wakifanya vitendo kadhaa viavyo akisi hisia zao, kama vile kumlaani Omar na kucheza ngoma. Marjaa Taqleed wa Kishia hawakubaliani na sherehe hizi. Pia wanazuoni wa Kishia wana pingamizi juu ya ushahidi na usahihi wa Hadithi hii, na pia wanadai kuwa maudhui yake yanakinzana na Qur'ani na Hadithi zingine. Maudhui ya Hadithi Hadithi au simulizi la "Rufi’a Al-Qalamu" ni Riwaya refu ya kihistoria na kidini inayochukua nafasi katika baadhi ya maandiko ya kale ya Kishia. [1] Na kulingana na simulizi za Hadithi hii ni kwamba; Siku ya tisa ya mwezi wa Rabi’u al-Awwal imeidhinishwa kama ni sikukuu ya maalumu, [2] ambapo katika kipindi hicho, makosa ya kibinadamu hayawekwi katika daftari za uhasibu wa kimaadili—yaani, hakuna rekodi za dhambi za wanadamu zinazorekodowa ndani ya siku hiyo. [3] Ufafanuzi uliotolewa juu kuidhinishwa siku hii kama ni siku ya Idi, ni kwamba; siku hii ndiyo siku ya maadhimisho ya tukio la kihistoria, la kuuawa kwa adui wa Mungu (Omar bin Khataab), mchukivu wa Imamu Ali (a.s), dhalimu na mnyang’anyi wa haki za Ahlul Bait (a.s) kwa makusudi. [4] Hivyo basi, kulingana na vyanzo vilivo ripoti Hadithi hii ni kwamba; simulizi hii imesimuliwa na Imamu Hassan al-Askari (a.s), aliyoinukuu kutoka kwa Mtume (s.a.w.w). [5]
Sherehe za Sikukuu ya Zahraa (Idu al-Zahraa) Makala Kuu: Mwezi Tisa Rabi’u al-Awwal Kwa kutegemea simulizi au Riwaya ya "Rufi’a Al-Qalamu", baadhi ya watu hushiriki katika sherehe za sikukuu inayoitwa "Idu al-Zahra", inayofanyika mwezi tisa mwezi Rabi’ al-Awwal, ambapo watu hao hujihusisha na vitendo kadhaa vinavyo akisi hisia zao, ikiwa ni pamoja na; kucheza kwa mtindo wa kupiga miguu ardhini, [6] kupiga makofi, na kumtusi Omar ibn al-Khattab. [7] Hata hivyo, wanazuoni wakuu wa kidini maulamaa wa Kishia, wakiwemo Marajii Taqleed (Mujitahidina au wanajitihadi), kama vile; Mirza Jawad Tabrizi, [8] Nasir Makarim Shirazi, [9] na Lotfollah Safi Golpayegani, [10] wameonesha msimamo wa wazi wa kabisa wa kukataa desturi hizi. Wakidhirisha msimamo wao huo, nasema kwamba mila hiyo haikubaliki na ni yenye napingana na kanuni msingi za mafundisho ya Kiislamu.
Vyanzo vya Hadithi Riwaya ya "Rufi’a Al-Qalamu" imerekodiwa na kunukuliwa katika vyanzo vya kihistoria vya Hadithi tangu karne ya tano ya Hijria na kuendelea, ikiwa ni pamoja na chanzo kinayotambulika kwa jina la “Majmu’ al-A’yad”, kilichoandikwa na Tabarani Nusairi. Naye ndiye kiongozi mkuu wa madhehebu ya Nusairiyya, ambaye alikuwa mmoja wa wafuasi wenye msimamo mkali wa kiitikadi (Kighulati), aliyeishi katika karne za nne na tano Hijria. [11] Aidha, Riwaya hiyo inapatikana katika kitabu kiitwacho Zawa’id al-Fawa’id, kazi ya Sayyid Ibn Tawus, mwanazuoni mashuhuri wa Kishia aliyejulikana kwa uzamifu wake wa kina katika maarifa ya kidini na kisufi (kiirfani), [12] na inapatikana pia katika kitabu kiitwacho Al-Muhtadhar, [13] kilichoandikwa na Hassan bin Suleiman Hilli, mwanafunzi wa Shahid al-Awwal. Allama Majlisi, ambaye ni mwanahadith mashuhuri wa karne ya kumi na moja ya Hijria, aliinukuu Riwaya hii kwa kina kutoka katika vyanzo viwili vya awali—Al-Muhtadhar [14] na Zawa’id al-Fawa’id— [15] katika kazi yake maarufu ya Bihar al-Anwar, ambayo ni moja ya ensaiklopidia muhimu za Hadithi za Kishia. Mapungufu ya Kiithibati na Kimaudhui ya Hadithi Hii
Mafaqihi, wataalamu wa elimu ya rijali (uchunguzi wa wasifu wa wasimuliaji wa hadithi), pamoja na watafiti wa upande wa madhehebu ya Kishia wamechukua msimamo wa kuikataa Hadithi ya "Rufi’a Al-Qalamu". Wamechukuwa hatua hii kwa kuwa haina ithibati kamili katika ushahidi wa mapokezi yake pamoja mapungufu katika maudhui yake, jambo linalodhoofisha uhalali wake. Mapungufu haya yamefafanuliwa kama ifuatavyo: 1. Shaka Juu ya Chanzo cha Riwaya: Wanazuoni wamesisitiza ya kwamba; Riwaya hii haijarekodiwa katika vyanzo vya msingi vya Kishia kama vile; Al-Kafi na Al-Tahdhib, ambavyo vinachukuliwa kuwa ndiyo vyanzo msingi vya mapema na vya kuaminika katika uwanja wa Hadithi. [16] Kwa upande mwengine ni kwamba; chanzo cha kwanza kinachohusishwa nayo ni kitabu cha madhehebu ya Nusairiyya, ambacho kiliandikwa katika karne za nne na tano Hijria, nacho ni kitabu kinawakilisha itikadi za kikundi chenye msimamo mkali wa kiitikadi (Kighulati). [17] Hii inaibua maswali makubwa kuhusiana na uhalali na ukweli wa kuwepo kwa riwaya hiyo. [18] Marajiu Taqlid (wanajitahidi) wakuu kama vile; Mirza Jawad Tabrizi na Nasir Makarim Shirazi, wameikanusha Riwaya hii kwa uwazi kabisa, wakisema kwamba; Riwaya hii haina msingi thabiti katika vyanzo vya kidini. [19] 2. Ukosefu wa Utambulisho wa Wasimulizi Wake: Baadhi ya wasimulizi wanaodaiwa kuwepo kwenye msururu wa wasimulizi wa riwaya hii hawajathibitishwa wala hawajulikana katika vyanzo vya elimu ya rijali (uchunguzi wa wasifu wa wasimuliaji wa hadithi), jambo ambalo linadhoofisha uaminifu wa mnyororo wa usimulizi wake. [20] 3. Ukinzani Wake na Mafundisho ya Qur’ani: Kulingana na maoni ya Nasir Makarim Shirazi, Riwaya hii inapingana na Aya za Qur’ani zinazosisitiza kuandikwa kwa matendo ya wanadamu bila kubagua tarehe fulani katika uandishi huo. Aidha, mafundisho ya Ahlul Bait (a.s) yanaelekeza watu kwenye maadili mema na kukataza utendaji dhambi, hali inayoiweka Riwaya hii katika mgongano wa wazi na kanuni msingi za Kiislamu. [21] Tafsiri ya Riwaya Sayyid Ibn Tawus (Rehema za Mungu ziwe juu yake), katika kitabu chake Zawa’id al-Fawa’id, alinukuu simulizi itokayo kwa Ibnu Abi al-Alaa Al-Hamdani Al-Wasiti na Yahya ibnu Muhammad ibn Huwaij Al-Baghdadi, ambao walisema: "Tulikuwa tukibishana kuhusiana na Ibnu al-Khattab, na tukakangaywa suala hilo. tukakubaliana, kulielekea Qum na kuonana na Ahmad ibn Ishaq al-Qummi, rafiki wa karibu wa Abu al-Hassan al-‘Askari (a.s). Tulipofika na kubisha hodi mlangoni kwake, mara akaja msichana mdogo wa Kiiraq (atokanaye nan chi ya Iraq). Tukamuulizia Ahmad ibn Ishaq al-Qummi, akatujibu akisema: ‘Yeye anasherehekea Idi yake, kwa kuwa leo ni siku ya Idi. Nikajibu kwa mshangao: ‘Subhanallah! Sikukuu za Washia ni nne tu: Idu al-Fitr, Idu al-Adha, Idu al-Ghadir, na Ijumaa.’ Binti akajibu: ‘Ahmad ibn Ishaq amesimulia kutoka kwa bwana wake, ya kwamba; Abu al-Hassan Ali ibn Muhammad al- Askari (a.s), amesema kwamba siku hii ni sikukuu, na ndiyo Idi yenye hadhi ya juu zaidi mbele ya Ahlul Bait (a.s) pamoja na wafuasi wao.’" Tukamwomba: "Atuombee ruhusa na umjulishe kuhusiana na kuwasili kwetu." Wanasema (wasimulizi wawili hawa):"Akaingia ndani, na kumwarifu, na akatutokea akiwa amevaa kikoi kiunoni mwake, akinukia harufu ya miski safi, huku akipangusa maji usoni mwake. Tuliistaajabia hali yake, akasema: ‘Msiwe na wasiwasi, nimejisafisha kwa ajili ya Idi. Tukajibu: ‘Kwani leo ni siku ya Idi?’ Akathibitisha kwa kusema: ‘Ndiyo’, naye alimaanisha siku ya tisa ya Rabi’ al-Awwal." Wanasema (wasimulizi wawili hawa): "Akatukaribisha nyumbani kwake na kutuweka kitato, kisha akasema: "Kwa hakika mimi, siku moja nilikwenda kwa bwana (Sayyid) wangu Abu al-Hasan (a.s) kwa njia ile ile ambayo ninyi mmekuja kwangu mimi hapa Surramanra’a (Samarraa). Nilipofika nilimwomba ruhusa ya kuingia, na nilipoidhinishwa, niliingia nyumbani kwake katika siku kama hii—yaani, tarehe tisa ya mwezi wa Rabi’ al-Awwal. Nilimudu Sayyid wetu (Amani iwe juu yake yeye pamoja na mababu zake), akiwa ametoa amri kwa kila mmoja kuvaa mavazi mapya kulingana na uwezo wake. Na mbele yake kulikuwa na chetezo cha kufukizia udi, huku akiwa anafukiza udi kwa mikono yake mwenyewe." Nikamwambia: "Tujibu kwa heshima ya baba zetu na mama zetu, ewe mwana wa Mtume wa Mungu, je, kuvaa nguo mpa katika siku hii hupelekea watu wa nyumba ya Mtume (Ahlul Bait) (a.s) kwa na furaha mpya?" Akajibu (a.s): "Siku gani yenye hadhi mbele ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), kuliko siku hii ya tarehe tisa ya mwezi wa Rabi’ al-Awwal? Hakika baba yangu (Amani iwe juu yake) alinisimulia akisema kwamba; Hudhaifa bin al-Yaman alimtembelea babu yangu, Mtume wa Mungu (s.a.w.w), katika siku kama hii. Katika matembezi hayo, Hudhayfa anasema: ‘Nilimwona Amiri Al-Muumina (a.s) pamoja na wanawe wawili (Hassana na Hussein) wakishiriki chakula pamoja na Mtume wa Mungu (s.a.w.w). Huku Amiru Al-Muuminina (a.s) akiwatazama Hassana na Hussein (a.s) kwa tabasamu, na kuwaambia: “Kuleni, baraka na furaha ya siku hii iwe juu yenu! Kwani siku hii ndiyo siku ambayo Mwenye Ezi Mungu atamwangamiza adui Yake na adui wa babu yenu. Na hii ndiyo siku ambayo Mwenye Ezi Mungu Mungu huyakubali matendo ya wafuasi wenu na wapenzi wenu (Mashia). Hii ndiyo ili siku ambayo neno la Mungu, Mtukufu, lisemalo: “فَتِلْكَ بُيُوتُهُمْ خاوِيَةً بِما ظَلَمُوا” ‘Zile basi ndizo nyumba zao zilizoporomoka kwa sababu ya udhalimu wao’ litakapo thibitika. Na hii ndiyo siku ambayo Firauni wa watu wa nyumba ya Mtume (Ahlu Al-Bait), dhalimu wao na mnyang’anyi wa haki zao, atakapo angamizwa. Na hii ndiyo siku ambayo Mwenye Ezi Mungu anayageukia matendo yao, na kuyafanya mavumbi yaliyotawanyika.”
Hudhaifa amesimulia akisema: "Nikamwuliza: ‘Ewe Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w)! Je, katika Ummah wako na miongoni mwa Masahaba wako, kuna wale ambao watavunja mipaka iliyowekwa na Mwenye Ezi Mungu?’" Mtume (s.a.w.w) akajibu: "Ndiyo, ewe Hudhaifa! Miongoni mwa wanafiki, mtu muovu amabaye ni Jibt (Omar bin Al-Khattaab) atachukua hatamu za uongozi juu yao. Atatumia ndoto za uongo kuwadanganya watu wa Ummah wangu, naye mabega yake yatachukua alama ya aibu (Dirratu al-Khizyi). Atawazuia watu kufuata njia ya Mwenye Ezi Mungu, akipotosha Kitabu Chake (Qur’ani), na kuharibu Sunna zangu. Atanyakua urithi wa kizazi changu, akijijengea (akijipamba) sifa za uwongo, na kudai ukuu kuliko kiongozi wa haki baada yangu. Atateka mali za watu kwa hila, kisha kuzitumia katika maasi dhidi ya Mwenye Ezi Mungu. Atanikadhibisha mimi, pia atamkadhibisha ndugu yangu na msaidizi wangu (Imam Ali), na atahusudu (atapinga) kwa chuki haki ya binti yangu (Bibi Fatima). Hapo Binti yangu atamlilia Mwenye Ezi Mungu Hazza wa Jalla (Mtukufu na Mweza), na Mwenye Ezi Mungu atamkubalia na kumjibu maombi yake katika siku kama hii ya leo!’" Hudhaifa aliendelea kusimulia akisema: "Nikamwambia: ‘Ewe Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w)! Omba kwa Mola wako amwangamize adui huyu ukiwa bado uhai!’" Mtume (a.s.w.w) akajibu: "Ewe Hudhaifa! Sitaraji kuharakisha maamuzi ya Mwenye Ezi Mungu Azza wa Jalla (Mtukufu na Mweza), ambayo tayari yameandikwa katika elimu Yake ya milele. Hata hivyo, nimemwomba Mwenye Ezi Mungu aijaalie siku ya kuangamizwa kwake, iwe siku ya tukufu kupindukia masiku mengine yote, ili iwe ni desturi na mila (siku kuu) kwa wale wanaonipenda mimi na wafuasi wa Ahlul Bait (Familia yangu) pamoja na wapenzi wawapendao wapenzi wa Ahlu Al-Bait." Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mweza akamjibu Mtume (s.a.w.w) kwa kumwambia: "‘Ewe Muhammad! Katika elimu Yangu ya awali na ya milele, nilijua kwamba wewe na Ahlul Bait wako mtajikuta katika majaribu ya kidunia, ukandamizwa wa wanafiki, na uonevu wa wanyang’anyi miongoni mwa waja wangu. Wale uliowapa ushauri wakakusaliti; wale uliowatendea wema wakakufanyia khiana (wakakughushi); wale uliowapatia amani wakakukataa; wale uliowaridhisha wakakukataa! Kwa hakika naapa kwa uweza Wangu na mamlaka Yangu, nitamfungulia kila mnyang’anyi wa Ali (a.s)—mteule wako wa kweli—milango elfu ya moto wa Jahannam, moto unaochomoza chini ya Filauki (Jina la Moto). Nitamchoma yeye pamoja na wafuasi wake kwa moto ambao hata Iblisi (Shetani) atakapouona moto huo atawalaani. Siku ya Kiyama nitamfanya mnafiki awe ni somo, kama vile watakavyokuwa Mafirauni wa Mitume na maadui wa dini katika uwanja wa malipo. Nitawakusanya wao, wafuasi wao, pamoja na madhalimu wote, na wanafiki, kisha nitawahukumu kwenye Jahannam wakiwa na macho ya hofu, aibu, na majuto. Wao watadumu hamo milele na milele!’" "Ewe Muhammad! Hakika msaidizi wako na mteule wako (Imam Ali), aliye katika daraja lako, atakabiliwa na majaribu makubwa kutoka kwa ‘Firauni’ wake na mnyang’anyi wa haki yake atakayemdhihaki, akipindua maneno Yangu, akinishirikisha katika uungu Wangu, na kuwazuia watu kufuata njia Yangu. Atakuja na atawatengenezea watu wa Ummah wako ndama (kama ndama wa Saamiri katika zama za Nabi Musa), akikanusha ukuu Wangu kwenye kiti changu cha enzi. Kwa hakika mimi, nimewaamuru Malaika Wangu walioko katika mbingu saba, pamoja na wafuasi wako na wapendwa wako, kusherehekea siku nitakayo muangamiza ndani yake. Nimewaagiza (Malaika hao) waiweke Kursi (Arshi) Yangu ya utukufu wangu karibu na Al-Bait al-Ma’mur wanisifu mimi, na kuwaombea msamaha wafuasi wako na wapendwa wako miongoni mwa wanadamu. Ewe Muhammad! Nimewaamuru Malaika wanaorekodi matendo kuinua kalamu zao siku hiyo na wasiandike makosa yoyote yale kutoka katika matendo ya watu katika siku hii, hiyo ni kutokana na heshima yako na ya mteule wako. Ewe Muhammad! Hakika mimi nimeifanya siku hii kuwa ni sikukuu kwa ajili yako pamoja na Ahlul Bait wako, na kwa wale waumini wote wanaowafuata wao ambao ni Mashia (wafwasi) wao. Na nimeapa kwa Uwezo Wangu Utukufu Wangu na Utkuu Wangu: Nitampenda yeyote anayeisherehekea siku hii kwa nia ya kupata thawabu. Nitakubali shufaa yake kwa watu wa familia yake Siku ya Kiyama. Nitamzidishia (nitambarikia) mali yake ikiwa atajijali yeye pamoja na familia yake. Na kila mwaka katika siku hii, nitawaokoa maelfu ya watu miongoni mwa wafuasi wenue na wapenzi wanu kutokana na moto. Nitajaalia juhudi zao zihimidiwe, makossa yao yasamehewe na amali zao njema zikubaliwe!’" Hudhaifa anasema: "Kisha Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w) aliondoka na kuingia nyumbani kwa Ummu Salamah (r.a). Na pale niliporudi, sikubakiwa na shaka yoyote ile kuhusina na yule aliyerejelewa na kutajwa kwa jina la “kafiri” (Omar). Na baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), niliposhuhudia kuzuka kwa uovu, kurejea kwa ukafiri, na kupotoshwa kwa dini. Yeye (Omar) Alijitayarisha kwa utawala, akapotosha mafundisho ya Qur’ani, akachoma nyumba ya ufunuo (Bait al-Wahyi), na kuanzisha mila potovu.
Alibadili mfumo wa dini, akakataa ushahidi wa Amir al-Mu’minina (a.s), na kumkanusha Bibi FAtima (a.s), binti wa bwana Mtume (s.a.w.w). Alinyakg’anya na kunyakua ardhi ya Fadak, akawapendelea Wayahudi, Wanasara na Wamajusi, na akamghadhibisha mpendwa wa bwana Mtume (s.a.w.w), yaani Bibi Fatimah (a.s). Alipindua sheria za Kiislamu, akapanga njama za kumuua Amir al-Mu’minin (a.s), na kudhihirisha ukatili wake. Aliharamisha yaliyohalalishwa na Mwenye Ezi Mungu na kuhalalisha yaliyoharamishwa.
Alikaribia kuamrisha watu watengeneze kupitia ngozi ya ngamia, akampiga kibao Bibi Fatima (a.s), akapanda mimbar ya bwana Mtume (s.a.w.w) kwa dhuluma (kinyume na sheria), akamzulia Amiru al-Mu’minin (a.s) kwa uongo, akapingana naye na kudharau rai zake." Hudhaifa akaendelea kwa kusema: "Mwenye Ezi Mungu akaikubali dua ya kiongozi wetu (Ali a.s) dhidi ya mnafiki huyu. Hatima yake ikatimia kwa mkono wa yule aliyemuangamiza—rehema za Mwenyezi Mungu zimshukie!" Hudhaifa anasema: "Baada ya tukio la kifo cha huyo mnafiki, nilikwenda kumtembelea Amir al-Mu’minin (a.s), nikimpongeza kwa kuuawa kwake, kuangamia kwa njia ile ya aibu na kulipizwa kwake kisasi. Naye (a.s) akaniambia: ‘Ewe Hudhaifa! Je, unakumbuka siku uliyotutembelea mimi, Mtume (s.a.w.w), na wajukuu wake (Imamu Hasan na Hussein) pale tulipokuwa tukila naye, siku ambayo Mtume (s.a.w.w) alikufahamisha utukufu wa siku hii? Nikajibu: ‘Ndiyo, ewe ndugu wa bwana Mtume (s.a.w.w)!’ Imam Ali (a.s) akasema: "Naapa kwa jina la Mwenye Ezi Mungu! Kwamba hii ndiyo siku ambayo Mwenye Ezi Mungu (s.w.t) ameyafariji macho ya watoto wa bwana Mtume (s.a.w.w). Kwa kweli mimi ninajua majina 72 ya siku hii!" Hudhaifa akasema: "Ewe Amir al-Mu’minin! Tafadhali nitajie majina ya siku hii ya tarehe tisa ya mwezi wa Rabiʿ al-Awwal." Imam Ali (a.s) akasema: “Ewe Hudhaifa! siku hii ni: • Siku ya Mapumziko • Siku ya Kupunguzwa Huzuni na Mateso • Ghadeer ya Pili • Siku ya Kufutwa kwa Makosa • Siku ya Kupokea Neema • Siku ya Kuinuliwa kwa Kalamu (Raf’u Al-Qalam) • Siku ya Sadaka (kutoa zawadi) • Siku ya Aqiqa • Siku ya Baraka • Siku ya Kulipiza Kisasi • Sherehe Kuu ya Mwenye Ezi Mungu • Siku ya Kubaliwa Maombi • Siku ya Kusimama Mbele ya Mwenye Ezi Mungu • Siku ya Uteuzi (Kuteuliwa) • Siku ya Sharti • Siku ya Kuvunjika Vikwazo • Siku ya Majuto ya Wadhalimu • Siku ya Kushindwa kwa Uovu (Siku ya Mashia Kuutoa Mwiba Wao) • Siku ya Kupotea Huzuni • Siku ya Ushindi • Siku ya Kujifunua (Siku ya Kujimwaga) • Siku ya Uwezo wa Mungu • Siku ya Kusamehewa • Siku ya Furaha kwa Mashia • Siku ya Kunywesha (Siku ya Kuondoa Kiu) • Siku ya Kurudi kwa Mwenyezi Mungu • Siku ya Zaka Kuu • Siku ya Idd ya Pili • Siku ya Njia ya Mwenye Ezi Mungu • Siku ya Kunywa Mateso • Siku ya Ridhaa • Siku ya Sherehe kwa Ahl al-Bait (a.s) • Siku ya Ushindi wa Wana wa Israili • Siku ya Kukubaliwa kwa Matendo ya Mashia • Siku ya Kutoa Sadaka • Siku ya Kuomba Ziada • Siku ya Kuuawa kwa Mnafiki • Siku ya Muda Maalum • Siku ya Furaha kwa Ahl al-Bait (a.s) • Siku ya Ushuhuda • Siku ya Wadhalimu Kutafuna Vidole Vyao • Siku ya Kuvunjiwa kwa Upotevu • Siku ya Fadhila (Chumo) • Siku ya Shahada (Kushuhudia) • Siku ya Kusamehe Waumini • Siku ya Usafi (Kujisafisha) • Siku ya Kupotea Mamlaka ya Mnafiki • Siku ya Uthatiti (Msimamo) • Siku ya Burudani (Mapumziko) kwa Waumini • Siku ya Mubahala • Siku ya Kujifakharisha • Siku ya Kubaliwa Matendo • Siku ya Kudhoofika (Kupwaya) • Siku ya Tunuku (Zawadi) • Siku ya Shukurani • Siku ya Kumsaidia Mdhulumiwa • Siku ya Ziara (Matembezi) • Siku ya Urafiki (Siku ya Kujenga Upendo) • Siku ya Kilio (Ukelele wa Kilio) • Siku ya Kuwasili • Siku ya Baraka • Siku ya Kufichua Bidaa (Uzushi) • Siku ya Kujiepusha na Makosa Makubwa • Siku ya Mwito (wa Mwitaji) • Siku ya Mawaidha • Siku ya Ibada • Siku ya Uislamu Hudhaifa akasema: "Kisha niliondoka kutoka kwa AmIr al-Mu’minin (a.s) huku nikijisemeza moyoni mwangu: ‘Kama nisingepata taufiki ya kutenda thawabu yoyote ile, isipokuwa kuwa na pendo wa kuipenda siku hii, basi ingalinitosha kunipa matumaini!’" Muhammad ibn Abi al-Alaa al-Hamadani na Yahya ibn Jariih wanasimulia wakisema: "Kila mmoja wetu alimkumbatia Ahmad ibn Is’haq (r.a) kwa heshima, huku tukisema: ‘Shukrani kwa Mwenye Ezi Mungu ambaye hakutukutanisha na mauti kabla ya kutufadhilisha kupitia baraka ya siku hii takatifu!’ Hapo tukaondoka kutoka kwake huku tukiisherehekea siku hii, kwa kwe hii ni siku ya Sherehe kwa Mashia. Huu ndiyo mwisho wa habari." [22]