Nenda kwa yaliyomo

Bismillahi al-Rahmani al-Rahim

Kutoka wikishia
Bismillah al-Rahmani al-Rahim

Bismillahi ( بسم الله الرحمن الرحيم) au Basmalah ( البَسْمَلَةَ) : Ni Aya ya Qur’ani inayo patikana mwanzoni mwa kila Sura, isipokuwa Suratu al- Tawba. Kuna Riwaya kadhaa zinazo elezea sifa za Aya hii; kati ya sifa zake ni kule kuhesabiwa Aya hii kuwa ni moja ya Aya bora na kubwa zaidi zilizoko ndani ya Qur’ani Tukufu.

Wanazuoni Waislamu wanaichukulia Bismillahi kuwa ni moja ya maneno na mbiu muhimu zaidi katika Uislamu na wanapendekeza isomwe mwanzoni mwa kila amali, hata mwa mazungumzo pia wamependekeza kusoma Bismillahi al-Rahmani al-Rahim.

Kulingana na fatwa za wanazuoni, ni haramu kugusa maandishi ya Bismillahi bila kuwa na wudhu. Pia, wakati wa kuchinja wanyama kisheria, ni lazima kusema Bismillahi.

Wanazuoni wa Imamia na baadhi ya wanazuoni wa Ahl as-Sunnah wanaamini kuwa; Bismillahi ni Aya katika kila Sura, Aya ambayo inabidi kuhisabiwa ni Aya huru na ni moja ya sehemu ya sura hiyo; lakini baadhi ya Ahlu al-Sunnah wanasema kuwa; Aya hii ni Aya huru tu katika Suratu ya Al-Fatiha na ni moja ya sehemu ya Sura hiyo, pia wako wengine wanaodhani kwamba; hata katika Suratu al-Fatiha, Bismillahi si miongoni mwa Aya huru ya Sura hiyo; badala yake husomwa mwanzo wa kila Sura (isipokuwa Sura ya Tawbah tu) kwa nia ya kutaka baraka na rehema za Allah.

Kulingana na baadhi ya wataalamu wa historia, Aya hii pamoja na Aya nyingine za Suratu al-Fatiha, kwa mara ya kwanza zilitafsiriwa kutoka Kiarabu kwenda Kifarsi na Salman al-Farisi. Tafsiri tofauti za “Bismillah al-Rahman al-Rahim” zinapatikana katika lugha Kifarsi, moja wapo ikiwa ni tafsiri isemayo: “Kwa jina la Mwenye Ezi Mungu Mrehemevu Mwenye kurehemu”.

Umuhimu wa Bismillah katika Utamaduni wa Kiislamu

Muhammad Jawad Mughniyya katika tafsiri ya Al-Kashif ameandika akisema: Baada ya shahada mbili, “Bismillah al-Rahman al-Rahim”, ndio kauli mbiu zaidi ya Waislamu, ambayo huwa ndio ufunguo wa kufungulia matamshi yao mapoja na matendo yao mbali mbali. [1] Kulingana na maoni ya Mortadha Mutahhari, ambaye ni mwanafalsafa na mtafiti wa Kiislamu, ni kwamba; sentensi hii ni moja ya kaulimbiu muhimu za Uislamu na ili isisahaulike, ni vizuri Waislamu kuandika maneno haya kwa kwa sanaa za michoro yenye kupendeza na kuweka kwenye kuta za nyumba zao, pia kuyasoma kwa sauti kubwa mwanzoni mwa kuanza shughuli zao. [2]

Inasemekana kwamba; moja ya mambo na tamaduni zilizo zoeleka nchini Iran, ambao zilikuwa zimezagaa miongoni mwa Waislamu wa nchi hiyo, ilikuwa kuandika sentensi ya “Bismillahi” juu ya jiwe au vigae (tiles), kisha kuweka juu ya milango ya nyumba zao ili kubarikiwa na kuzilinda familia zao kutokana na maafa. [3] Kutokana na matumizi mengi ya “Bismillah” mwanzoni mwa shughuli mbali mbali, sentensi hii katika lugha utamaduni wa Kifarsi, huwa inatumika kwa maana nyengine kinyuma na maana alisi, Wafarsi huitumia sentensi hii katika kutoa baadhia ya amri au kuwakaribisha wageni, hivyo basi badala ya wao kusema; “tadhadhali karibu”, “harakakisha” au “anza”, huwa wanasema “Bismillah”. [4] Pia, mwanzoni mwa ripoti za tasnifu (thesis) na vitabu, huanzwa kwa “Bismillah al-Rahman al-Rahim” au tafsiri yake (Be name Khodaa Bakhshandeye Merabaan). [5]

Inasemekana kwamba, hapo awali bwana Mtume (s.a.w.w) alikuwa akiitumia sentensi isemayo “Biimika Allahumma”, ambapo mwanzoni mwa utume wake, aliitumia ibara hiyo mwanzoni mwa barua zake na pamoja na mambo mengine yanayo fanana na hilo, [6] aliendelea kufanya hivyo mpaka pale illipoteremshwa Aya isemayo: “وَ قَالَ ارْكَبُوا فِيهَا بِسْمِ اللَّهِ مَجْرَاهَا وَ مُرْسَاهَا”. [7] Ilipoteremshwa Aya hii akabadili na kuanza kutumia sentensi isemayo: “Bimillahi بِسْمِ اللَّهِ”, aliendelea kutumia ibara hiyo hadi ilipoteremshwa Aya ya 110 ya Suratu al-Israa, ambapo alianza kutumia ibara isemayo: “Bismillahi al-Rahmani بسم الله الرحمن”, akabaki kuitumia ibara hii mpaka pale ilipoteremshwa Aya isemay: “إِنَّهُ مِنْ سُلَيْمَانَ وَإِنَّهُ بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ”. [8] Ilipoteremshwa Aya hii, Mtume Muhammad (s.a.w.w) akaachana na ibara hizo na kuanza kutumia ibara mpya isemayo: “بسم الله الرَّحمن الرَّحیم” (Bismi al-Lahi a-Rahmani al-Rahim) kiukamilifu. [9] Baadhi wanaamini kwamba “Bismillah ar-Rahman ar-Rahim” ndio Aya ya kwanza ilioshuka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) ikishikamana na Aya za Suratul-Alaq. [10]

Pia wakati mwengine “Bismillah ar-Rahman ar-Rahim”, huitwa “Basmalah” [11] au “Tasmiyah” [12].

Bismillahi ni Ufunguo wa Kila Jambo Wafasiri wanasema; Kule waja wa mwenyezi Mungu kutumia “بسم الله الرحمن الرحیم”mwanzoni mwa kila jambo, ni kwa ajili ya kumkumbuka Mwenye Ezi Mungu na kufulingamanisha Naye kila tendo walitendalo waja hao. [13] Kulingana na maoni ya Sayyid Muhammad Hussein Tabataba’i katika tafsiri ya Al-Mizan, ni kwamba; Mwenye Ezi Mungu meianza Qur’ani tukufu kwa jina lake lenye heshima zaidi, ili kuyafanya maneno yake yawe na alama au muhuri unao muashiria Yeye. Pia, kwa kufanya hivyo, amewafundisha waja wake kuwa; vitendo vyao na maneno yao vianziwe kwa jina lake Yeye, ili maneno na matendo yao yawe na muhuri wa Kiungu ndani yake. [14]

Maana ya Bismillah

Baadhi ya wafasiri wana maoni ya kwamba; herufi Ba ilioko katika neno "Bismi" ina maana ya kianzio "primitive"; Yaani pale mtu asemapo: “Bismillahi” ina maana kwamba ameanza kazi yake kwa jina la Mwenye Ezi Mungu [15] Kundi jingine linasema kwamba; herufi hiyo ya "Ba" haina maana maalum katika uwepo wake kwenye neno hilo; Badala yake, kusema Bismillahi mwanzoni mwa maneno na matendo yetu, kuna maana ya kichocheo kinachotoa na kutoa msukumo wa kulikumbuka jina la Mwenye Ezi Mungu ndani ya matendo na amali hizo kwa lengo la kulibarikiwa na Allah. [16] Kundi jingine la wafasiri wameichukulia herufi “Ba” ilioko kwenye neno hilo kuwa na maana ya “kuomb msaada”. [17] Kwa hiyo basi, pale tusemapo: «بسم‌الله», huwa tunamaanisha kunaomba msaada kwa jina la Mwenye Ezi Mungu. [18] Pia baadhi ya wafasiri wa Kishia [19] wanakubaliana na maana hii kutokana na uwepo wa kunukuu za Riwaya kutoka kwa Maimam (AS), zinazounga mkono maana hiyo. [20] Baadhi ya wafasiri wengine wanasema kwamba; kwa vile ndani ya Qur'ani, huwa hakuna marudio ya Aya fulani kujirejea kwa maana moja, "بسم الله الرحمن الرحیم" iliko katika kila Sura za Qur'ani, kila wakati itabidi kuwa na maana maalum na tofauti kabisa, hivyo basi kila "بسم الله الرحمن الرحیم" itabidi kufasiriwa kulingana na maudhui ya Sura hiyo tu. [21] Katika Tafsir "Ayashi", kuna nukuu ya Riwaya itokayo kwa Imamu Sadiq (a.s.) kuhusiana na tafsir ya Bismillah, Riwaya hiyo yaeleza kwamba; Herufi ya "Ba" ilioko katika neno "Bismi" ina maana ya "Bahaa'u al-Llahi" kwa maana ya "Nuru ya Mwenye Ezi Mungu". Pia kulingana na Riwaya hiyo, herufi ya "Sin" ina maana ya"Sana'u a-Llahi", kwa maana ya "Uadhamu wa Mungu", na "Mim" imefasiriwa kama ni "Majdullah", yenye maana ya ukuu wa mwenye Ezi Mungu." [22]

Sheria za Fiqhi Kuhusiana na Bismillahi

Mafiqihi wametoa wametoa hukumu za “Bismilahi” katika milango tofauti ya kifiqhi, miongoni mwayo ni; Milango wa tohara, sala, nikaah (ndoa), uwindaji na uchinjaji, Sadaka pamooja na Kula na Kunywa. Baadhi hukumu za kifiqhi kuhusiana na “Bismillahi” ni kama ifuatavyo:

  • Kugusa Bismillahi: Kulingana na maoni ya mafaqihi maarufu wa Kishia, ni haramu kugusa bila udhuu Bismillahi iliyo andikwa mahala fulani, hii ni kutokana na kuwa Bismillahi ni moja ya Aya za Qurani [23] na kwamba, ndani yake mna majina na sifa za Mwenye. [24] Pia ni haramu kwa mwenye janaba kugusa maandishi ya Bismillahi. [25]
  • Bismillahi katika Qur’ani: Kulingana na makubaliano ya mafaqihi wa Shia, Bismillahi ni sehemu na ni Aya katika Sura zote za Qur’ani, isipokuwa Suratu al-Tawba tu, hivyo basi ni wajimu kuisoma Aya hii katika Sura zisomwazo wakati wa Sala. [26]
  • Uwindaji na Kuchinja kihalali (kisheria): Kulingana na fatwa za mafaqihi, ni kwamba kupiga (kusoma) “Bismillah” ni miongoni mwa masharti ya utekelezaji wa amali ya kuchinja kihalali (kisheria). [27] Pia katika suala la uwindaji, wakati wa kumtuma mbwa kumshika mnyama fulani au kumuinda kwa kupiga mshale, ni lazima kupiga “Bismillah” kabla ya kumtuma mbwa huyo au kupopoa mshale huo, na iwapo mtu ataacha kusoma “Bismillahi” kwa makusudi, bila shaka nyama ya mnyama huyo itaharamika na hauitakuwa halali kuliwa. [28]

Vile vile ni sunna Kupiga “Bismillah” wakati wa kutawadha, [29] mwanzo wa tendo la ndoa [30] na pia kabla ya kula chakula na kabla ya kunywa vinywaji. [31]

Je, Bismillah ni Aya ya Kujitegemea?

Kulingana na taarifa kutoka kwa Rashidreza (aliyeishi kati ya mwaka 1282 na 1354 Hijiria), ambaye ni mfasiri wa Kilebanon, ni kwamba; Kwa kuwa Bismillah ni sehemu ya Aya ya 30 ya Suratu al-Naml, Waislamu wote wanakubaliana kwamba, Bismillahi ni sehemu ya Qurani; lakini kuna tofauti ya maoni kuhusu ikiwa Aya hii inachukuliwa kama ni Aya ya kujitegemea mwanzoni mwa Sura nyingine za Qur’ani. Alusi, mmoja wa wafasiri wa Kisunni, katika tafsiri yake ya Roh al-Ma’ani, ametoa mitazamo kumi kuhusiana na suala hili, ambayo baadhi yake ni kama ifuatavyo:

  • Mtazamo wa madhehebu ya Imamiyyah; Baadhi ya Masahaba na Tabi’ina, akiwemo Shafi’i na wengi wa wafuasi wake, pamoja na baadhi ya wasomaji wa visomo saba vya Qur’ani, akiwemo Asim na Al-Kisa’I, wanaamini kwamba; Bismillah ni Aya ya kujitegemea na inajumuishwa katika Sura zote za Qur’ani, isipokuwa Suratu al-Tawba tu ambayo haina Bismillahi ndani yake. [35] Baadhi ya hoja zao husiana na hilo ni pamoja na:
  1. Ijma’a (makubaliano ya pamoja) ya Masahaba yaliofokiwa katika ukusanyaji wa Msahafu wa kwanza, ambapo “Bismillah” imeandikwa mwanzoni mwa kila Sura zilizomo ndani ya Msahafu huo, isipokuwa Suratu al-Tawba.
  2. Hadithi kutoka vyanzo vya pande zote mbili -Kisunni na Kishia- zinanukuu ya kwamba; Bwana Mtume (s.a.w.w) na Maimamu wa Kishia wakiitambua “Bismillah” kuwa ni Aya ya kujitegemea na ni sehemu ya kila Sura miongoni mwa Sura za Qur’ani Tukufu, na kama ingelikuwa Bismillahi si Aya au si sehemu ya Qur’ani, bila shaka ingelikuwa ni wajibu kwa bwana Mtume (s.a.w.w) kuweza wazi suala hilo, kwani kukaa kimya kwake kutapelekea kupotea kwa Umma wote wa Kiisalamu. [38]
  3. Maimamu na wanazuoni kadhaa akiwemo;
  • Malik bin Anas, Abu Hanifa na wafuasi wake, Abu Omar pamoja na Ya’qub bin na Ishaq kutoka kwa wasomaji wa Basra wakiambatana na baadhi ya wanazuoni wengine, wote kwa pamaoja wanachukulia “Bismillah” kuwa ni Aya ya pekee inayo jitegemea, ambayo imekuja kwa ajili ya kutoa baraka na kuwa ni ufunguo wa kufungulia Sura za Qur’ani, na pia kuweka mpaka baina yake na Sura nyengine, [39] na haihisabiwi kuwa ni sehemu ya Sura yoyote ile isipokuwa katika Aya ya 30 ya sura An-Naml, yaani ni sehemu ya Aya ya Sura hiyo tu peke yake, na si Aya wala si sehehemu ya Aya ya Sura nyengine yoyote. [40]
  • Ahmad bin Hanbal anasema, Hamza amabye ni miongoni mwa wasomaji saba wa Qur’ani, pamoja na baadhi ya wasomaji wengine, wanaamini kwamba; Bismillah ni Aya ya pekee katika Suratu Al-Fatiha tu na inahesabiwa kuwa sehemu ya sura hiyo. [41]

Baraka na Faida za Bismillahi Kuna barak chungu nzima kuhusiana na “Bismillahi” zilizo orodheshwa ndani ya vyanzo vya tafsiri ya Qur’ani pamoja na Riwaya kutoka pande zote mbili; za Shia na Sunni. Qurtubi katika tafsiri yake anamnukuu Imam Ali (a.s) akisema kwamba; Bismillah ni dawa ya kila ugonjwa na msaidizi wa kila dawa. [42] Kulingana na Hadithi ilioko katika tafsiri ya Ayyashi inayo mnukuu Imam Ridha (a.s), ni kwamba; Aya hii ndiyo Aya yenye hadi zaidi na ndiyo Aya adhimu zaidi katika Quriani. [43] Pia katika baadhi ya riwaya, imeelezwa kuwa; kuiandikwa Bismillah kwa hati nzuri, ni miongoni mwa sababu za kupata msamaha na rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, [44] na kuisoma kwake hupelekea kupata ukombozi na wokovu kutokana na moto wa Jahannam. [45] Katika moja ya hadithi imeelezwa kwamba; siri zote za vitabu vyote vya mbinguni zimo ndani ya Quran, na kila kitu kilicho ndani ya Quran kimo ndani ya Suratu al-Fatiha, na kila kitu kilichmo ndani Suratu al-Fatiha kimo ndani ya Bismillah. [46]

Nafasi ya Yake Kwenye Kazi za Sanaa

Miaka nenda na miaka rudi, Bismillahi imekuwa ni mojawapo ya Aya ambazo kuandika kwake kumekuwa na umuhimu mkubwa kwa wasanii wa kaligrafia, kuna kazi mbali mbali ndani ya historia ya Waislamu zilizo andikwa kwa kutumia aina tofauti za maandishi. [47] Pia sanaa hii ya uchoraji wa Bismillahi inaeonekana katika sanaa ya kuchora wa kauri (tiles), ikiwa ni moja ya sanaa za mapambo na usanifu wa Iran. Sanaa ya uchoraji wa Bismillahi ni moja ya kazi maarufu katika fani ya useremala, uchoraji ambao unaonekana katikz kazi mbali mbali; ikiwemo milango, mihrabu za misikiti, na maeneo mengine matakatifu. [48] Aidha, kazi mbalimbali za uchongaji na kuandika Basmala zimebuniwa na wasanii wa Kiislamu katika ukataji na usanifu wa mbao na uandishi wa njia ya michimbo kwenye vyombo vya mapambo na fakhari. Wakati mwengine Bismillahi hupatikana katika mashairi na fasihi za Kifarsi, ambapo mara kwa mara huonekana ktumika ndani ya mishororo ya shairi hayo, [49] pia na mara nyingine utakuta kuna baadhi ya mashairi yalio tungwa kwa ajili ya kuhimiza matumizi ya Bismillahi. [50] Katika fasihi ya Kifarsi, istilahi kama “morghe bismil” humaanisha kuku aliye chinjwa na “morghe niime bismil” inamaanisha kuku nusu roho (asiye na afya), pia “bismilgaah” humaanisha machinjioni. [51] Tafsiri ya Kifarsi ya Bismillahi al-Rahimani al-Rahim Inasemekana kwamba; kwa mara ya kwanza kabisa, Bismillahi pamoja na Aya nyengine za Suratu Al-Fatiha zilitafsiriwa kwa Kifarsi na Salman Farsi kupitia ombi la wasemaji wa lugha yaKifarsi. [52] Yeye aliifasiri Aya hiyo kama ifuatavyo: “Be name Yaazdan Bakhshaawand”, [53] ibara ambayo kwa Kiswahili ni: “Kwa jina la Mungu Mrehemevu.” Baadhi ya tafsiri nyingine za Aya hii kwa Kifarsi ni kama ifuatavyo:

  • Isfara’ini, mfasiri wa Kisunni wa karne ya tano Hijria: “Ibtidaa kardam be name Khodaye Qaadir Aafariinesh khaaliqaan, Khaahaane ruzidaadane khaliqaan, Khaahaane aamurziidane mutii’aan” Ibara ambayo kwa Kiswahili ni kwamba: “Nimeanza kwa jina la Mungu Mwenye uwezo wa kuumba viumbe, Mtakaye kuwapa riziki viumbe, Mtakaye kusamehe watiifu.” [54]
  • Rashid al-Din Abu al-Fadl Maybudi, mfasiri wa Qurani katika karne ya sita Hijria: “Be name Khodaawandi Jihaandari Dushmanpawar be bakhshayandegi wa Dustbakhshai be mehrabaani” “Kwa jina la Mola Mlezi wa ulimwengu, Mwenye kwastahamilia maadui kwa hisani zake, mwenye kuwarehemu waja wema wake kwa upendo.” [55]
  • Abu al-Futuhu al-Razi, mfasiri wa Shia katika karne ya tano Hijria: “Be name Khadaa Mehrabaan bisiyaar Bakhshande” [56] “Kwa jina la Mungu mwenye upendo na Mtoaji wa rehema nyingi mno.”
  • Mullah Husayn Waa’idh Kashifiy, mfasiri wa Shia katika karne ya tisa Hijria: “Be name Khadaa sezaaye parastesh wa Bakhshande bar khalqe be wujuud wa hayaatbakhshiidan wa Bakhshayande barayeshaan be baqaa wa zindedaashtan be qudrat wa hikmat az aafaat muhaafizat nemuudan” [57] “Kwa jina la Mungu Anayestahiki ibada na Mtoaji wa rehema kwa viumbe wake kwa kuwapa uhai na kuwalinda dhidi ya maovu.”
  • Tafsiri ya Tabari ambayo ni moja ya tafsiri za zamani zaidi za Qurani kwa Kifarsi: “Be name Khodaaye Mehrabaan Bakhshayande” “Kwa jina la Mungu mwenye upendo na Mrehemevu.” [58]
  • Katika tafsiri za Qurani za sasa (yaani karne ya kumi na nne na kumi na tano Hijria), kumekuwa na tafsiri mbalimbali za Aya hii, ambapo tafsiri isemayo: “Be name Khodaawand Bakhshandeye Merabaan” “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu” ni moja ya tafsiri maarufu zaidi za Aya hii. [59]

Tafauti Kati ya Neno Rahmani na Rahimu Rahmani رحمان na Rahimu رحیم: ni sifa mbili za Mwenyezi Mungu ambazo kwa maoni ya wafasiri wengi, [60] zimepatikana kutokana na neno “rahma.” [61] Wafasiri wengi [62] wamesema kwamba; “رحمان” ni rehema maalum ya Mwenye Ezi Mungu [63] inayo maanisha rehema ya kijumla, ambayo inajumuisha waja wote ndani yake, iwe ni makafiri au waumini. Na Sifa ya “رحیم” inaashiria rehema endelevu na ya kudumu ambayo inawahusu waja waumini tu peke yao. [64] Kwa maoni ya baadhi ya wafasiri, upande wa kijumla wa sifa hii ya Rahmaaniyya رحمانية ya Mwenye Ezi Mungu kwa waja wake wote kwa jumla, ni kwamba yeye ndiye aliyewaumba na ndiye anaye waruzuku. [65] Na ule upande wa pekee wa Rahiimiyya رحیمية (ambayo ni rehema) yake maalumu kwa waumini tu, ni kwamba yeye anawapa wao mafanikio katika maisha haya duniani na pia kuwapa Pepo katika maisha ya Akhera, pamoja na kusamehe dhambi zao. [66]

Tafsiri ya Kiirani (za Kiroho au za Kisufi)

Katika maandiko na tafsiri za kiirfani au kiroho, kumetolea tafsiri maalumu za kiirfani kuhusiana na herufi na vokali za Bismillahi. [67] Baadhi ya wafasiri na wanazuoni wa fani hii, katika tafsiri zao kuhusiana na Aya hii wamesema kwamba; Mwenyezi Mungu ameumba viumbe vyote kupitia herufi ya “Ba” ilioko katika Bismillahi. [68] Ibnu ‘Arabi alilinganisha umbo la “Ba”, nukta, na vokali zake na milimwengu mitatu; akisema kuwa umbo la “Ba” ni ulimwengu wa Malakuti (Mithal, ulimwengu usio na kiwiliwili), nukta yake ni ulimwengu wa Jabaruti (‘Aalamu al-‘Aqli au ulimwengu wa akili), na vokali zake ni ulimwengu wa Shahada (‘Aalamu al-Shahaada au ulimwengu wa viwiliwili). [69] Abdulrazzaq Kashani pia katika tafsiri yake, ameihisabu herufi ya “Ba” ilioko katika “Bismillah” kama ishara ya akili ya kwanza au asili ya kwanza yaani kiumbe wa kwanza kabisa kuumbwa na Mwenye Ezi Mungu. [70] Kulingana na Mulla Husayn Wa’idhi Kashifiy katika kitabu chake “Jawahiru al-Tafsir,” herufi ya “Alif” inaashiria Dhati takatifu ya Allah, na kutokana na kuwa ni herufi ya kwanza kabisa katika alfabeti, inafaa kuwa ni ishara inayo muashiria Mwenye Ezi Mungu kama ni asili ya vitu vyote, na kutokana na kutokuwa na nukta, inafaa kuwa ni kiashirio cha upweke kamili wa Mwenye Ezi Mungu ambao umepekeka kutokana na aina zote za mafungamano na mahusiano. [71] Katika baadhi ya maandiko na tafsiri za kiirfani, neno “Rahmani” limeelezwa lina maana ya Muumbaji na mtoaji wa ukamilifu wa kuvikamilisha viumbe vyote, kulingana na hekima na uwezo wa viumbe hivyo ulivyo. [72] Na “Rahim” imeelezwa kumaanisha Mtoaji wa ukamilifu maalum wa kiroho kwa wanadamu. [73]

Rejea

Vyanzo